diocesedemahaginioka

Prière du Centenaire en kiswahili

 SALA  KWA AJILI YA MIAKA MIA MOJA   YA UTANGAZAJI YA HABARI NJEMA

 KWA DIOCEZI YA MAHAGI-NIOKA 

1912-2012

 

Mungu Baba, kwa mapendo yako isiyo na mwisho, ulimtuma Mwana wako Yezu kwa kutuokoa na kutufanya wana wako. Roho Mtakatifu alitugeuza tuwe wana wako kweli, imekuwa sasa miaka miya moja.

 

Kuusu sacramenta zilizopokelewa mara ya kwanza kwetu kwa miaka elfu moja mia kenda na kumi na mbili, sisi waana wako, wanaume na wanawake wa Diocezi ya Mahagi-Nioka, tunakutolea sala hii kwa moyo mnyenyekevu :

 

Aksanti kwa kututumia watangazaji ya Habari Njema ya wokovu wakisaidiwa na msaada ya Mama wetu Bikira Maria, Malkia wa Afrika. Kazi wale watangazaji waliofanya, uliwaokowa watu wengi katika miaka hii miya moja, ukiwavuta wafuate Mwana wako. Kati yao, uliwachagua maaskofu, mapadri, mafrera na bikira, wakatekista na wakristu waliosaidia kueneza vema Enjili na kazi mbalimbali, wakiishi makusudi ubatizo ya uito wao. Kwa hayo yote, ee Mungu, tunakushukuru, kwa moyo wote. Aksanti kwa kubadilisha roho yetu mzima kwa mwangaza ya Enjili.

 

Uwabarikie wamisionari waliotuhubiri Neno la Mungu: maaskofu, mapadri, watawa na wakristu waliojitoa kwa kuwasaidia. Uwapokee katika mwanga wako wale wote waliotutangulia na kifo; hasa waliohuuwawa na nguvu kwa Aba, Mahagi, Biringi, na wengine wote pia.

 

Utusaidie tusherehe na utukufu wote yubileo ya miaka moja ya utangazaji. Wamisionari ya mwanzo walianza, wengine walioizidisha, na sisi tufanye nguvu kwa kuiendelesha milele.

Kwa kukosa kujitolea kwa kazi yetu mbaya, kwa makosa yetu yaliorudisha nyuma maendeleo ya Ufalme wa Mungu, na 

ukamilishi ya jamaa ya Mungu katika Diocezi yetu, Bwana, utuhurumie!

 

Kwa ubaguzi wetu, kwa ukosefu ya undugu tukitegemea  ujamaa yetu ndogo, kwa njia ya ukabila, kwa jina ya jimbo letu, kwa roho yetu ya kujitenga na wengine, kwa kufunga roho kwa wengine tukijitafuta sisi wenyewe, kwa kuwazarau wengine, kwa kuwa na niya pia tabia mbaya kwa wengine, kwa kuwa na chuki, Bwana, Utuhurumie!

 

Bwana, utusaidie ili mwisho ya hii miaka miya moja ulio mwanzo ya miaka mingine itupatie kujitoa na nguzu zaidi, kadiri tulizoea, kwa kuendelea katika mwangaza kubwa zaidi.

 

Utufanyizie tuwe jamaa ya Mungu na roho wazi na kujikaza pamoja, tusikilizane kati yetu, tuwe na huruma kati yetu, tupendane, mkono mkononi tuendelee pamoja kwa uwema.

 

Utusaidie Habari Njema iingii katika maisha yetu kweli kweli na itubadirishe ili ishara ya Ufalme wa Mungu ionekane katika maisha yetu.

 

Tunakuomba msaada yako, ee Bwana, ili Eklezia yako isimame imara kwetu, iwe moja, takatifu, katholiki na yenyi msinzi kwa mitume.

 

Bikira Maria Mtakatifu, Malkia wa Africa, utuombee!

Watakatifu maishaidi ya Uganda, mutuombee!

Mtakatifu Joséphine Bakhita, utuombee!

Mwenyi heri Maria-Klementina Anuarite, utuombee!

Mwenyi heri Isidore Bakanja, utuombee!

Mwenyi heri Francisko Spoto, utuombee!

 

 

« Repartons du Christ,

Unique  Sauveur »

 

 

 

 

 

 

 

 

 



22/08/2012
0 Poster un commentaire

Inscrivez-vous au blog

Soyez prévenu par email des prochaines mises à jour

Rejoignez les 11 autres membres